Ni nini umuhimu wa zawadi katika penzi na jinsi zawadi inavyoweza kuboresha na kustawisha penzi lenu
Mengi tumezoea kuishi kimazoea na kutegemea zawadi toka upande mmoja bila ya mwenza mwingine kuonyesha upendo kwa njia ya zawadi


Kama tunavyojua hakuna raha hapa duniani kama kupendwa na mwenza wako kuonyesha anakupenda pia kwa
kuonyesha thamani ya mpenzi wako lazima umpende kwa dhati kwa matendo mbalimbali ili naye afurahie mahusiano mliyonayo.
Kijana lazima utambue jinsi ya
kulilinda na kulitunza penzi lako kwakupendaye,na njia mojawapo ya kulitunza penzi ni kutoa ZAWADI.
Ninapoongelea zawadi
namaanisha ya aina yoyote ile ambayo unahisi itamfanya mwenzi wako ahisi na kutambua pendo lake kwako.
Unaweza ukanunua ua japo wengi mnasema maua ni ya nyuki tu lakini ni njia moja wapo ya kuonyesha upendo ,kadi yenye maneno mazuri ya mahaba,viatu,gauni au kitu chochote na kwa mwanaume inaweza ikawa perfume boxer na chochote ambacho unadhani mpenzi wako atafurahia
na kitakuwa kumbukumbu nzuri kwa mwezi wako,hata kama
anapanga kukusaliti,akiangalia zawadi ile ama kuikumbuka basi lazima nafsi itamsuta na kujikuta akiacha kukusaliti na kubaki akikuwaza wewe.
Jifunze jinsi ya kuuteka moyo wa
mwenzi wako kwa kumnunulia zawadi .Maana unakuta watu wengine wako katika mahusiano au ndoa kwa muda wa miaka mitatu na kuendelea ,kwao hawajui hata zawadi ni nini kwa mwenzi wake zawadi yake anawaza fedha na
mapenzi tu.
Mara nyingi zawadi inafaa kuwa kitu maana hakiishi thamani kwa mara moja kama pesa mjali mpenzi wako kwa zawadi japo mara moja kwa mwezi hasa kwa kipindi cha valentines au hata kununulia kitu ambacho
amekimiss na anakipenda zaidi hapo lazima utamfurahisha sana kwani hata kama ukimpa pesa zitaisha lakini zawadi ataikumbuka daima.
Zawadi ni kitu muhimu sana kuliboresha penzi
la mwenzi wako
,kwani zawadi hushawishi na kusababisha akuamini kuwa unampenda,na pia zawadi huweka kumbukumbu nzuri ndani ya akili na kamwe kumbukumbu ya zawadi haifutiki mapema kama ilivyo kumbukumbu ya pesa,maana waliompa pesa ni wengi lakini uliyemnunulia shati na perfume ni wewe.